Jumatatu , 2nd Mei , 2016

Mchezaji nyota wa timu ya Free State Stars ya nchini Afrika Kusini, Mrisho Ngassa ameanza mazoezi ya taratibu baada ya kuanza kupona kutokana na upasuaji wa goti aliofanyiwa.

Mshambuliaji Mrisho Ngassa.

Kutoka nchini Afrika Kusini, Ngassa amesema kwamba ameanza mazoezi kuhakikisha anajiweka fiti na ni mazoezi ya taratibu sana.

Ngassa amekaa takribani mwezi nje ya uwanja akiuguza maumivu ya goti na baadaye alifanyiwa upasuaji huo ambao ulikwenda vizuri kwa mujibu wa madaktari.

Kiungo huyo raia wa Tanzania mwenye kasi, amesema ana imani kubwa mambo yataenda vizuri baada ya muda si mrefu na kurejea tena dimbani.