Jumanne , 2nd Feb , 2021

Michuano ya Ligi ya kikapu nchini Marekani NBA, itaendelea alfajiri ya kuamkia kesho kwa michezo sita, lakini mchezo miwili inayotazamiwa kufuatiliwa na wengi ni kati ya Brooklyn Nets dhidi ya LA Clippers na ule wa Golden State Warriors dhidi ya Boston Celtic.

Wachezaji wa Brookyn Nets, kuanzia kushoto, James Harden, Kevin Durrant na Kyrie Irving.

Mchezo wa Brooklyn Nets unatazamiwa kuwa wenye upinzani mkali na kusisimua kutoka na wakali hao kuwa na wachezaji nyota kama vile James Harden, Kyrie Irvinng na Kevin Durrant ambao watakaribisha vinara kutoka upande wa Magharibi LA Clippers.

Los Angeles Clippers, watajivunia kiwango bora cha mchezaji wake nyota, Kahwi Leonards na Paul George ambao huenda wakawa fiti kukipiga saa 9:30 alfajiri ya kuamkia kesho tarehe 3 Februari 2021 baada ya kukosekana kwenye michezo miwili iliyopita kwasababu za kiafya.

Brooklyn Nets hawana rekodi nzuri mbele ya LA Clippers katika miaka 21 iliyopita kwenye NBA, hivyo watahitaji kulipa kisasi kwa kupata matokeo mazuri kufuta uteja na kwenda nafasi ya pili kwa kuwashusha Milwaukee Bucks.

Ikumbukwe kuwa Brooklyn Nets imecheza michezo 22, ikifungwa 13 na kufungwa 9 ukiwemo mchezo wa mwisho waliofungwa na Washington Wizards kwa alama 149 kwa 146 ilhali LA Clippers wamecheza michezo 21, wakishinda 16 na kufungwa michezo 5 pekee.

Mchezo mwingine wa kuvutia ni ule wa Golden State Warriors watakapokipiga na Boston Celtic saa 12:00 alfajiri ya kuamkia kesho tarehe 3 Februari 2021. Golden watajivunia fomu bora ya nyota wake Stephen Curry wakati Boston wakitegemea ukali wa Jayson Tatum.

Golden State Warriors wamecheza michezo 20, wakishinda 11 na kufungwa michezo 9 wakati Boston Celtic wamecheza michezo 18, wakishinda 10 na kufungwa 8.

(Mchezaji nyota wa Boston Celtic, Jayson Tatum.)

Wawili hao wanaviwango vya kupanda na kushuka hivyo watachuana vikali kupata alama zaidi.