Jumatatu , 21st Feb , 2022

Kocha wa Simba SC, Mhispaniola Pablo Franco Martin amesema sare yaliyoipata ugenini dhidi ya timu ya US Gandermarie ya Niger ni matokeo muhimu sana kwa upande wao kwenye michuano hiyo ya Shirikisho Barani Afrika.

(Kocha wa Simba SC, Pablo Franco Martin)

Simba ilishuka dimbani Jumapili ya Februari 20, 2022 kutupa karata yake ya kwanza ugenini na kufanikiwa kusawazisha bao dakika za lala salama lililofungwa na Bernard Morrison dakika ya 84 akitokea benchi.

Sare hiyo imemfanya Pablo aseme kuwa, “Hii alama tuliyopata ni muhimu sana kwetu. Kuja ugenini na kupata alama ni jambo kubwa."

Naye Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya klabu ya Simba, Salim Abdallah almaarufu ‘Try Again’ ameshukuru wanachama na mashabiki wa Simba SC kwa kuipambania na kuiombea timu yako mpaka kupata matokeo ya sare.

Try Again pia, amewasifu benchi la Ufundi kwa jitihada zao katika mechi hiyo licha ya changamoto zote walizopitia ikiwemo kuchelewa kuwasili nchini Nigera pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa nchini humo.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Sasa Simba SC inajiweka tayari kusafiri kuelekea nchini Morocco kuifuata klabu ya RS Berkane kwenye mchezo wa mzunguko watatu wa michuano hiyo inayotaraji kuchezwa Februari 27, 2022.

Simba ndiye kinara wa kundi D akiwa na alama 4, Berkane wapili akiwa na alama 3 sawa na ASEC Mimosas mwenye alama 3 na kumuacha US Gandermarie kushika mkia akiwa na alama moja aliyiopata kwenye sare dhidi ya Simba SC.