Novak Djokovic ameshinda taji la wazi la Ufaransa baada ya kumchapa Andy Murray kwa seti 3-6 6-1 6-2 6-4 kwenye viwanja vya Roland Garros.
Mserbia huyo mwenye umri wa miaka 29, anakuwa mtu wa kwanza kumiliki mataji yote manne ya Grand Slam kwa mchezo wa tenesi, tangu Rod Laver aliyeshinda mwaka 1969.
Murray mwenye umri wa miaka 29, anakuwa Muingereza wa kwanza kcheza fainali ya Paris, tangu mwaka 1937.

