Alhamisi , 3rd Dec , 2020

Nyota wa klabu ya Yanga, Said Ntibazonkiza amesema atahakikisha anajituma kama ilivyo kawaida yake ili kupigania nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha wanajangwani.

Nyota mpya wa Yanga, Said Ntibazonkiza enzi akikipiga katika anga la Ulaya.

Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini usiku wa kuamkia leo, Ntibazonkiza raia wa Burundi amesema amefarijika kwa kupata mapokezi makubwa kutoka kwa wanachama na viongozi ambao wameonyesha imani kubwa dhidi yake.

''Kwakweli nimefarijika kwa mapokezi makubwa, nakuja katika timu ambayo ina hadhi ya ubingwa, sitaki kuongea mengi bali shughuli itaonekana uwanjani.

Yanga nimeifuatilia , ni timu nzuri na wachezaji wenye uwezo, naamini kwa pamoja tutaungana ili kuiletea mafanikio timu yetu yenye kiu ya ubingwa'' alisema Ntibazonkiza.

Nyota huyo, ambaye kwa mechi za hivi karibuni katika timu yake ya Taifa ya Burundi, amefunga bao 4 katika mechi 3, anatajwa kuwa ni ingizo jipya ambalo litaongeza chachu ya kupachika mabao katika safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inasuwasuwa.