Alhamisi , 29th Dec , 2022

Msafara wa wachezaji 19, benchi la ufundi na viongozi wameondoka Dar Es Salaam mchana wa leo kuelekea Morogoro, kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.

Yanga itakuwa wageni wa Mtibwa, Disemba 31,2022, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Manungu Complex, majira ya saa 10:00 Jioni.

Wachezaji waliosafiri leo ni, Djigui Diarra, Erick Johora, Shomari Kibwana, Bakari Mwamnyeto, Yanick Bangala, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Gael Bigirimana, Zawadi Mauya, Salum Abubakari, Jesus Moloko, Farid Mussa, Dickson Ambundo, David Bryson, Tuisila Kisinda, Yusuph Athumani, Clement Mzize, Stephane Aziz Ki na Fiston Mayele