Odhiambo ataiweza Biashara United?

Jumanne , 4th Mei , 2021

Patrick Odhiambo Liwowo raia wa Kenya ametambulishwa kuwa kocha mpya wa klabu ya soka ya Biashara United ya ligi kuu soka Tanzania bara.

Patrick Odhiambo akitambulishwa na uongozi wa Biashara United

Odhiambo anachukua nafasi ya Mkenya mwenzake Francis Baraza aliyetimukia timu ya Kagera Sugar kwa kile kinachoaminika ni kupandiwa dau, baada ya kuifundisha timu hiyo kwa takribani miaka miwili kwa mafanikio makubwa.

Kocha huyu ambaye amepata kuifundisha Gor Mahia akiwa kocha msaidizi, kwa sasa alikuwa anafundisha timu ya Home Boys ya Kakamega atalazimika kumalizia msimu huu kisha kuanza msimu ujao katika filosofi yake ikiwemo usajili litakuwa jukumu lake la moja kwa moja.

Odhiambo anakuwa kocha wa 6 wa kigeni katika ligi kuu Tanzania Bara, wengine ni Didier Da Rosa (Simba) Mohamed Nasreddine Nabi (Yanga) George Lwandamina (Azam) Mathias Lule (Mbeya City) Francis Baraza (Kagera Sugar) na Patrick Odhiambo (Biashara United ).

Takwimu za Biashara United hadi sasa ambapo Odhiambo anajiunga na timu ni nafasi ya 4, alama 44 michezo 28, kushinda michezo 12 sare 8 kupoteza 8 magoli ya kufunga24 na kufungwa 23.