Jumanne , 26th Oct , 2021

Ole Gunner Solskjear anatarajiwa kuendelea kuifundisha Klabu ya Manchester United licha ya kipigo walichokipokea kutoka kwa Liverpool.

Ole Gunner Solskjear

Licha ya tetesi za kutimuliwa kwake huku Antonio Conte akihusishwa,imedaiwa kuwa Uongozi unatarajia kujikita zaidi katika kuboresha hali iliyopo kuliko kumtimua kocha huyo.

Kipigo cha bao 5-0 kilisababisha maumivu makali kwa Klabu hiyo, huku ikiwa ni muendelezo wa matokeo mabaya kwani katika mechi nne za EPL wamejikuta wakikusanya alama moja pekee.

Katika mazungumzo yake, baada ya mchezo wa siku ya Jumapili, Ole Gunner alinukuliwa akisema wamepambana kwa pamoja kwa muda mrefu lakini wanakaribia kushindwa huku akisisitiza kipigo cha 5-0 kilikuwa ni kibaya zaidi katika kazi yake.

Ole anatarajiwa kuendelea kukinoa kikosi cha Manchester United ambacho mwisho wa juma kitakabiliana na Tottenham Hotspurs lakini pia ana kibarua kizito dhidi ya Manchester City kwenye muendelezo wa michezo iliyo mbele yake siku za karibuni.