Jumatatu , 26th Apr , 2021

Zikiwa zimesalia siku 88 kabla ya kuanza rasmi michuano mikubwa na mikongwe ya Olympiki tarehe 23/7/2021 Tokyo Japan, kamati ya kuratibu mashindano hayo imesema wapo katika hatua ya mwisho kuona uwezekano wa idadi ya mashabiki watakaoruhusiwa kuingia viwanjani.

Rais wa kamati ya maandalizi ya Olympic Tokyo 2020 Seiko Hashimoto

Rais wa kamati ya maandalizi bwana Seiko Hashimoto amesema ''tunatarajia kukutana kabla mwezi huu haujaisha kujadili kiwango cha mashabiki watakao ruhusiwa kuingia viwanjani lakini kwa haraka nachoweza kusema kutakuwa na mashabiki''

''Tutakaa na wenzetu wa Serikali,pamoja na watu wa kamati ya International Olympic Commitee 'IOC'mamlaka mbalimbali kutafuta suluhu ya jambo hili mwisho wa siku tunaamini tutapata muafaka''aliongeza

Mashindano haya ya mwaka huu yanatarajiwa kuanza tarehe 23/07/2021 na kumalizika 8/08/2021 pamoja na kutumia logo ya Tokyo 2020 kufuatia kuhairishwa kwa mashindano haya mwaka jana kutokana na janga la Corona.

Mashindano haya makongwe , yenye umri wa miaka 125 yanatazamiwa kuhusisha michezo tofauti tofauti 339 huku mchezo kivutio sana ikiwa ni riadha