Ijumaa , 3rd Sep , 2021

Kuelekea kilele cha Tamasha la Simba day, itakayofanyika siku ya September 19, mabingwa wa nchi Simba Sports Club, wamezindua kauli mbiu, inayosema 'One team, One dream' huku wakimalizia kwa kusema 'asubuhi tu twendeni wenye nchi '.

Kaimu Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga akizungumza jambo kupitia EA Radio.

Pia klabu ya Simba imezindua jezi zao mpya zitakazo tumika katika msimu wake mpya ujao w mwaka 2021-2022 na kutoa punguzo la bei kwenye jezi hizo kwa mashabiki wake watakao nunua tiketi za tamasha la Simba day kwenye maduka ya mdhabuni wao Vunja bei.

Sanjari na utambulisho wa kauli mbiu, Uongozi wa Simba kupitia kwa Kaimu Msemaji wake Ezekiel Kamwaga umeweka wazi viingilio vya uwanjani kuelekea Tamasha la Simba day litakalofanyika kwenye dimba la Benjamin William Mkapa, ambapo jukwaa la mzunguko itakuwa Shilingi elfu 5, tofauti na mwaka jana ilikuwa elfu 7.

VIP B na C itakuwa elfu 20 na VIP A tiketi zitauzwa laki 2 ambayo itaambatana na kupata ofa ya jezi pamoja na kofia, chakula cha mchana na usafiri wa kwenda na kurudi utakao sindikizwa na jeshi la polisi.

Kamwaga ametoa masikitiko yake kwa kulaani vikali kitendo cha kuvujisha jezi mpya za msimu ujao badala ya kungoja siku rasmi ya uzinduzi wa jezi hizo ambao ulipangwa kufanyika siku ya jumamosi ya Septemba 4 makau huu.

Akijibu swali kutoka kwa waandishi wa habari, Kamwaga amesema kuwa timu watakao cheza nayo kwenye Tamasha la simba day ni Mabingwa wa Afrika zaidi ya mara tatu lakini hakuitaja timu hiyo.