
Jil Teichmann wa Uswizi (kushoto) wakipongezana na Naomi Osaka (kulia) baada ya mchezo wao wa mzunguko watatu kumalizika kwa Jil kupata ushindi na kutinga hatua ya rob fainali mchana wa leo Agosti 20, 2021.
Baada ya kichapo hicho, Mwanadada Naomi Osaka mwenye umri wa miaka 23 amesema, “Nilikuwa na matarajio makubwa lakini, hakukuwa na kingine cha ziada ambacho ningefanya kushinda mchezo huu”.
Licha ya kufungwa na kushindwa kutinga robo fainali, Osaka amesema amekuwa mwenye furaha kwani amesaidia kuchangia dola za kimarekani 24, 200 sawa na milioni 56 na zaidi ya laki moja za kitanzania kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi nchini Haiti nyumbani kwa baba yake mzazi.
Kwengineko, Mcheza tenisi anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora nchini Australia na mshindi wa mashindano ya Wimbledon Open, Ashleigh Barty raia wa Autralia amemtoa bingwa mtetezi wa mashindano hayo, Victoria Azarenka kwa kumfunga 6-0 na 6-2 na kutinga hatua ya robo fainali.
Nyota mwingine aliyetinga robo fainali ni Angeliqque Kerber mjerumani aliyeshinda Grandslam mbili baada ya kumfunga Jelena Ostapenko wa Latvia kwa 4-6, 6-2 na 7-5 na kurekodi ushiriki wake wa kumi kwenye mashindano hayo.
Mkali kutoka Jamhuri ya Czech, Petra Kvitova amemfunga Ons Jebeur wa Tunisia kwa 6-1 na 6-2 na kuungana na nyota hao manguli wa Tenisi kwa upande wa wanawake.