Ijumaa , 10th Jul , 2020

Bodi ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza imetanabaisha kuwa kumekuwepo na maamuzi yasiyo sahihi matatu ya penati yalifanywa na waamuzi wasaidizi wa video VAR katika michezo yote mitatu ya Alhamisi,

mwamuzi akihakikisha tukio la utata wa penati kupitia VAR.

Bruno Fernandes alizawadiwa mkwaju wa penati na kufunga katika mechi ambayo Manchester United ilishinda 3-0 dhidi ya Aston Villa.

Raia huyo wa Ureno alionekana kumkanyaga mchezaji wa Villa Erki Konza ingawa VAR iliamuru adhabu ielekezwe kwa upande wenyeji wa mchezo huo.

Katika mchezo mwingine James Ward-Prowse alizawadiwa penati kwa madai Andre Gomez alimchezea madhambi katika eneo la hatari ingawa marudio ya video yanaonyesha mchezaji huyo aliaguka kirahisi,licha ya mkwaju huo kugongwa mwamba,lakini mechi ilimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mechi nyingine iliyozua utata ni ya Tottenham dhidi ya Bornemouth ambapo mshambuliaji Harry Kane aliangushwa kwenye eneo la hatari na Joshua King wa Bournemouth lakini waamuzi hawakutoa penati kwa vijana wa Jose Mourinho na mchezo ulimazika kwa suluhu.

Premier League imesema Man United na Southampton wasingepewa penati, lakini Tottenham ndiyo walistahili kupewa penati.

Akiliongelea hilo kiungo wa zamani wa Everton, Tim Cahill, amesema kunahitajika mchezaji mstaafu kuwepo karibu na wanaoangalia VAR ili kutoa ushauri kabla ya maamuzi .

'' Nafikiri hiyo ingewasaidi kabisa, kutambua mienendo”.Wakati mchezaji anapojiangusha unaweza kuhisi hilo.'' Alisema mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Australia.

Kumekuwa na mkanganyiko kwenye mechi za ligi kuu, ambapo mkuu wa waamuzi Mike Riley alipunguza matumizi ya viangalizi kwa sababu ilikuwa inapoteza muda.