Alhamisi , 14th Jan , 2021

Kocha wa PSG Mouricio Pochetino amaeshinda taji lake la kwanza katika maisha yake ya ukocha, baada ya kikosi cha chake kuifunga Olympique Marseille mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali wa French Super CUP, lakini pia amemshukuru kocha wa zamani wa kikosi hicho Thomas Tuchel.

Pochetino ameshinda taji lake la kwanza kwenye maisha yake ya ukocha

Maboa ya PSG kwenye mchezo huo yalifungwa na Moura Icardi dakika 39 na Neymar Jr alifunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 85 yalitosha kumpa Pochetino taji lake la kwanza katika maisha yake ya ukocha na bao la kufutia machozi la Marseille lilifungwa na Dimitri Payet dakika ya 89.

 

Baada ya mchezo huo kkumalizika pochetino alisema

"Nataka kuwashukuru wachezaji, mkurugenzi wa michezo Leonardo na Nasser Al-Khelaifi Rais, Pia natambua mchango wa Thomas Tuchel na wafanyikazi wake, ambao wametuwezesha kucheza mechi hii."

 

Pochetino amejiunga na mabingwa hao wa Ufaransa mwezi huu ikiwa ni kibarua chake cha kwanza tangu alipofutwa kazi na Tottenham ya England mwezi Novemba 2019, akichukua mikoba ya kocha mjerumani Thomas Tuchel na mchezo huo wa fainali ulikuwa ni mchezo wake wa 3 tangu aanze kukionoa kikosi hicho cha matajiri wa jiji la Paris.

 

Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 48 amewahi kuvifundisha vilabu vya Espanyol ya Hispania Southampton na Tottenham zote za England, mafanikio yake makubwa ilikuwa ni kuifikisha Tottenham kwenye fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu wa 2018-19 ambapo walifungwa na Liverpool kwenye mchezo wa fainali.