Jumamosi , 17th Nov , 2018

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amekutana na nyota wa Barcelona Lionel Messi huko Dubai ambapo wawili hao walionekana kuwa na mazungumzo ya muda mrefu kitu ambacho kimezua mjadala kuwa huenda mmoja wao anamshawishi mwenzake kuhama timu.

Messi na Pogba wakiwa kwenye Mgahawa mmoja huko Dubai

Wawili hao walisikika wakiongea kwa lugha ya Kihispania huku moja ya maneno yaliyonaswa ni Pogba kumwambia Messi juu ya wimbo waliokuwa wakiimba kwenye timu ya taifa ya Ufaransa juu ya Ngolo Kante kumthibiti Messi kwenye mechi ya Kombe la dunia 2018 Urusi.

Hata hivyo Messi alimjibu Pogba kuwa kuhusu wimbo huo sio kweli ni uongo na utani tu huku akicheka kuonesha hana tatizo na hilo.

Wawili hao waliendelea na maongezi wakionekana kuwa na utulivu wa hali ya juu kitu amnacho kinaacha maswali mengi kuwa walikuwa wanaongea nini.

Wapo wanaosema huenda Paul Pogba alikuwa anamshawishi Messi kuhamia Manchester United lakini wapo wanaodhani Messi amemshawishi Pogba kukamilisha tetesi zilizopo kuwa huenda akajiunga na Barcelona.

Pogba na Messi wote hawapo kwenye majukumu ya timu za Taifa Pogba akiwa ni majeruhi huku Messi akiendelea na mapumziko yake ya muda mrefu ambayo amechukua kuwa nje ya timu ya taifa.