Wachezaji wa PSG na kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer
PSG haikuwa imepoteza mchezo wowote wa ligi ya Ufaransa 'Ligue 1' katika mechi zake 20 za mwisho za ligi hiyo hadi hapo jana ilipofungwa mabao 2-1 na Lyon, mabao ya Lyon yakifungwa na Moussa Dembele na Nabil Fekir huku bao la PSG likifungwa na Angel Di Maria.
Ikumbukwe kuwa baada ya kumalizika kwa mchezo wa Leicester City na Manchester United jana Jumapili, kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer alisafiri hadi nchini Ufaransa kuutazama mchezo wa PSG.
"Solskjaer lazima atakuwa na furaha na alichokiona hapa, tulianza vyema mchezo lakini baadaye tulipoteza umiliki wetu na hatukuwa vizuri katika kipindi cha kwanza", amesema Silva.
"Lakini msiwe na wasiwasi na sisi, Jumanne ijayo Jijini Manchester itakuwa ni mashindano mengine, mazingira mengine na tunatakiwa kufanyika kazi ya ziada sisi wenyewe ili kuonesha kitu kipya", ameongeza Silva.
Manchester United na PSG zitakutana Jumanne ya wiki ijayo katika mchezo wa Klabu bingwa Ulaya katika uwanja wa Old Trafford, ambapo Man United imeshinda mechi 9 kati ya 10 za hivi karibuni.






