Ijumaa , 15th Oct , 2021

Mshambuliaji wa Uingereza, Raheem Sterling amesema atafikiria kuondoka katika klabu ya Manchester City, iwapo atapata nafasi ya kuhamia nje ya nchi ya EPL.

Raheem Sterling akionyesha makeke yake dimbani

Licha ya kuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha timu yake ya Taifa iliyoshiriki katika michuano ya Ulaya msimu wa 2020, nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 ameendelea kupata wakati mgumu kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Pep Guardiola msimu huu.

Baada ya kufunga mabao 30 katika michezo 51 msimu wa 2019/2020, Sterling alifanikiwa kufunga mabao 14 tu katika msimu uliopita na ameanza mara mbili tu kwenye Ligi Kuu msimu huu.

''Ikiwa kungekuwa na fursa ya kwenda mahali pengine ili kupata muda zaidi wa kucheza ,nadhani ningekuwa huru wakati huu''Raheem Sterling .

Mshambuliaji huyo alijiunga na Manchester City akitokea Liverpool mwaka 2015 kwa ada ya uhamisho kiasi cha paundi milioni 49 ambapo sasa amebakisha miaka miwili katika Mkataba wake ambao unamuweka Etihad .