Alhamisi , 22nd Mei , 2025

Nyota wa FC Barcelona mbrazil Raphinha ameongeza mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2028.

Raphinha mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na msimu bora katika kikosi hicho ambapo amechangia mabao 27 akifunga mabao 18 na assist 7 katika mechi 35 za Laliga msimu huu.

Licha ya mafanikio hayo pia ameisaidia klabu yake kuchukua ubingwa wa ligi kuu nchini Hispania, Super cup pamoja na Copa del rey.