
(kikosi cha Dynamo kyiv kikiwa kimebeba ujumbe wa kupinga vita)
Michuano hiyo haikurejea baada ya mapumziko ya miezi mitatu ya msimu wa baridi wa mwezi Desemba ambayo ilitarajiwa kuendelea mwezi huu wa april, lakini sasa haitaendelea tena kufuatia uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.
Shakhtar Donetsk ndio walikuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na pointi 47, ikiwa ni pointi mbili mbele ya Dynamo Kyiv waliokua nafasi ya pili na lama 45 wakati ligi hiyo inakwenda mapumziko kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa mwisho wa michezo ya ligi hiyo, Taarifa kupitia kwenye tovuti ya shirikisho la soka nchini ukraine ilisema kwamba Msimamo wa ligi hiyo UPL ulioishia tarehe 24 Februari 2022 ndio utakuwa msimamo wa mwisho wa msimu huu na hakuna washindi watakaotunukiwa zawadi.
Taarifa hiyo pia ilithibitisha kuwa tume maalum imeundwa kujadili kama kutakua na uwezekano wa kuwepo kwa msimu ujao w aligi hiyo. Shakhtar Donetsk na Dynamo Kyiv, ambao wanashikilia mataji 29 ya ligi soka nchini Ukraine, hivi karibuni wamecheza michezo ya kirafiki kutafuta fedha za kuwasaidia watu walioathiriwa na mapigano ya kivita yanayoendelea nchini ukraiane.