Ijumaa , 5th Dec , 2014

Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es salaam RD,kimewasilisha orodha ya wasimamizi watakaousika katika Mbioza Uhuru zinazotarajiwa kufanyika Jumapili ya Desemba saba mwaka huu Viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam,Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini RT,Suleiman Nyambui amesema wamepanga eneo husika ammbapo mbio hizo zitaanzia na zitakapoishia.

Nyambui amesema kwa ajili ya kuboresha mbio hizo,wametuma barua kwa Chama cha Riadha cha nchini Kenya RK,ili kuweza kupata wanariadha wa nchi hiyo kwa ajili ya kushiriki mbio hizo na bado wanasubiri majibu.