Alhamisi , 11th Jan , 2024

Kamati ya waamuzi ya Zanzibar imemaliza utata ikisema mwamuzi wa mchezo wa Singida Fountain Gate dhidi ya Simba SC mechi ya nusu fainali ya pili, Nasri Salum 'Msomali' hakuwa sahihi kuwapa shambulizi la kona wekundu hao.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Waziri Shekha amesema baada ya kikao kilichofanyika leo Januari 11, 2024 kupitia ufanisi uliofanywa na Msomali na wasaidizi wake wamegundua kwamba mwamuzi huyo hakuwa sahihi kwenye uamuzi wake huo wa kuwapa kona Simba.

Shekha amesema kosa hilo ni la kibinadamu kwani waamuzi nao hufanya makosa ambapo wamebaini ndio kosa pekee alilofanya Msomali ni kwenye mchezo huo wa jana usiku.