Yanga mabingwa NBCPL 2025/26
Katika msimu huu, Yanga walionyesha kiwango cha juu kwa kucheza soka la kuvutia, kukusanya pointi muhimu na kuonyesha uthabiti dhidi ya wapinzani wao Simba.
Hata hivyo ushindi huo haukuwa wa furaha zaidi kufuatia Jeraha mbaya la kuvunjika mguu alilolipata mshambuliaji wao Pacome Zouzoua dakika ya 45 baada ya kufanyiwa rafu.
Kwa kutwaa ubingwa huo, Yanga wameendelea kuthibitisha kuwa ni miongoni mwa vilabu vikubwa na vyenye mafanikio zaidi nchini Tanzania. Sasa macho ya mashabiki yanaelekezwa kwenye michuano ya kimataifa ambapo huko wameonekana wakisuasua baada ya kuishia katika hatua ya makundi kwa misimu miwili mfululizo








