Rekodi ya Azam FC na Ruvu Shooting ligi kuu

Jumamosi , 9th Mar , 2019

Klabu ya Azam FC imefurahia ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya JKT Tanzania, ilioupata jana usiku kwenye mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex.

Wachezaji wa Ruvu Shooting kushoto na Azam FC kulia.

Azam FC kupitia taarifa yake imewapongeza wachezaji wao kwa kujituma na kupata matokeo hayo ambayo sasa wao ndio wanashikilia rekodi ya kupata ushindi mnono zaidi kwenye Ligi Kuu msimu huu. 

Wanalambalamba hao wamevunja rekodi ya Ruvu Shooting ambao waliwapiga magoli 6-2 Mwdui FC kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa wiki kadhaa zilizopita.

Baada ya ushindi huo sasa Azam FC na Ruvu Shooting ndio timu mbili zilipata ushindi mkubwa zaidi kwenye ligi mpaka sasa.

Azam wapo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 57 kwenye mechi 27 huku Ruvu Shooting wakiwa katika nafasi ya 10 wakiwa na pointi 35 kwenye mechi 30.