Jumanne , 27th Apr , 2021

Hatua ya Nusu fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya inaanza kutimua vumbi hii leo kwa mchezo wa nusu fainali ya kwanza, ambapo Real Madrid ya Hispania watakuwa nyumbani katika dimba la Alfredo Di Stefano kuwaalika wa Chelsea ya England.

Chelsea haijawahi kupoteza mchezo dhidi ya Real Madrid

Toni Kroos na Eden Hazard wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha leo kwa upande wa Madrid lakini mabingwa hawa wa kihistoria wataendelea kumkosa nahodha wao Sergio Ramos kutokana na majeruhi.

Wachezaji wengine WA Real Madrid watakao kosekana ni Ferland Mendy, Lucas Vazquez na Federico Valverde ambao wana maambukizi ya Corona.

Kwa upande wa Chelsea wataendela kumkosa Matteo Kovacic ambaye anasumbuliwa na misuli, na huyo ndio mchezaji pekee mwenye majeruhi.

Hii ni nusu fainali ya nane kwa chelsea kwenye mashindano haya ikiwa ni mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote nchini England lakini wanacheza kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014.

Mara ya mwisho Real Madrid kucheza nusu fainali ya michuano hii ilikuwa msimu wa 2017-18

Kwa upande wa Real Madrid wanacheza nusu fainali ya kwanza tangu 2017-18 ambapo walitwaa ubingwa msimu msimu huo.

Hii itakuwa ni mara ya nne timu hizi zinakutana kwenye michuano ya vilabu barani Ulaya ambapo kwenye michezo mitatu iliyopita Chelsea wameshinda mara 2 na sare mchezo mmoja, hivyo Madrid hawajawahi kushindi dhidi ya Chelsea na mara ya mwisho kukutana ilikuwa mwaka 1998 kwenye mchezo wa UEFA Super Cup.