Jumanne , 26th Oct , 2021

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika kupitia tovuti yake ya Cafonline.com imethibitisha kuwa bado uamuzi wa mechi ya marudiano kati ya Ahly Tripoli na Biashara United haujatolewa.

Kikosi cha vijana wa Biashara Mara United

Leo saa nane mchana droo ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika itafanyika kule Cairo Misri kunako makao makuu ya CAF, ambapo timu 16 zilizofuzu raundi hiyo ya pili zitapangwa na timu 16 zilizotolewa kwenye ligi ya mabingwa Afrika.

Hata hivyo kwasasa orodha ya CAF CC ina timu 15 tu ambapo timu 1 ya 16 itatokana na uamuzi wa CAF kuhusiana na hatma ya mechi ya Ahly Tripoli na Biashara United.

Timu zilizofuzu ni RS Berkane(Morocco),JS Kabylie (Algeria), Enyimba (Nigeria) ,SC Sfaxien (Tunisia), JS Saoura (Algeria), Pyramids (Misri), Al Masry (Misri), Gor Mahia (Kenya), Marumo Gallants (Afrika Kusini), Coton Sport (Cameroon), Orlando Pirates (Africa Kusini), Red Arrows (Zambia).

Nyingine ni DC Motema Pembe,(DR Congo), Binga Fc (Mali), CD Inter clube (Angola), Tusker (Kenya), Hearts of Oak (Ghana), Stade Malien (Mali), LPRC Oilers (Liberia),US Gendarmerie Nationale (Niger), Al Itthad (Libya),, APR (Rwanda).

Vilabu vingine vilivyofuzu hatua hiyo ni pamoja na AS Maniema Union(DR Congo),TP Mazembe (DR Congo), Simba(Tanzania), Rivers United(Nigeria), ASEC Mimosas (Ivory Coast), AS Otoho( Congo), FC Nouadhibou(Mauritania), Royal Leopard (Eswatini), Zanaco (Zambia.