
Makamu wa kwanza wa Rais wa RT William Kallage amesema, mashindano ya Riadha ya Vijana chini ya Miaka 20 ya Afrika Mashariki na Kati (EAAR) ndio yamewapa tena uenyeji mara baada ya kuonekana kusimamia kwa umakini mashindano hayo japo wao kama waandaaji walikumbana na changamoto mbalimbali zilizochangia timu wenyeji kushindwa kufanya vizuri zaidi.
Kallage amesema, mashindano ya vijana chini ya miaka 20 yaliyohitimishwa Aprili 30 mwaka huu yameonyeshwa mafanikio makubwa ambayo yanaonyesha bado ipo nafasi kwa Tanzania kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali makubwa zaidi.
Mashindano ya Riadha ya Vijana chini ya Miaka 18 ya (EAAR) yalianza kutimua vumbi Aprili 29 na kuhitimishwa Aprili 30 yakishirikisha nchi 11 huku wenyeji Tanzania wakishika nafasi ya sita kwa ujumla katika mashindano hayo.