Alhamisi , 2nd Jun , 2022

Klabu ya Real Madrid ya Hispania imethibitisha kumsajili beki Antonio Rudiger akiwa mchezaji huru akitokea katika klabu ya Chelsea ya England. Rudiger raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 29 atasaini mkataba wa miaka 4 na Real Madrid.

Antonio Rudiger

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Real Madrid Rudiger atatambulishwa rasmi Jumatatu Juni 20, 2022. Na ataongea mbela ya waandishi wa habari.

Antonio Rudiger anajiunga na Real Madrid akiwa mchezaji huru baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya na Chelsea mapema mwanzoni mwa mwaka huu. Lakini hali ilikuja kuwa ngumu zaidi yeye kusalia Chelsea baada ya aliyekuwa mmiliki wa timu hiyo Roman Abromovich kuwekewa vikwazo na Serikali ya Uingereza kwenye mali zake zote anazomiliki na kupelekea Chelsea kuzuiliwa kusajili au kuwapa wachezaji mikataba mipya.

Beki huyo wa kati kisiki ameitumikia the Blues kwa kipindi cha miaka 5 amecheza michezo 203 amefunga mabao 12. Alijiunga na timu hiyo ya London mwaka 2017 akitokea katika klabu ya AS Roma ya nchini Italia, ameshinda makombe 5 akiwa na The Blues ikiwemo klabu bingwa baran Ulaya, UEFA Super Cup, klabu bingwa Dunia, Europa League na FA Cup.