Ijumaa , 16th Dec , 2016

Klabu ya Azam FC imesema mchezaji Farid Mussa anatarajiwa kuondoka muda wowote kuanzia sasa kuelekea nchini Hispania mara baada ya kukamilika kwa taratibu zote na huenda safari hiyo ikawa mwezi Januari mwakani.

Farid Musa

 Afisa habari wa klabu hiyo Jaffary Iddy Maganga amesema kilichokuwa kikisubiriwa ni vibali vya Farid kufanya kazi nchini Hispania na siyo kweli kwamba klabu hiyo ilikuwa ikimbaia.

"Waliokuwa wanasema tunamzuia Farid kwenda Hispania, kwanini hawajiulizi ni kwanini tulimruhusu aende kufanya majaribio, mchakato ulikuwa unaendela ikiwemo kupata vibali vya kazi, sasa kila kitu kiko tayari na ataondoka muda wowote kwenda kujiunga na klabu yake mpya ya Tenerife" amesema Maganga

Kwa upande wake Farid Mussa amethibitisha, kila kitu alichokuwa anasubiria kimeshakamilika na anachosubiria kwa sasa ni muda wa kuondoka kuelekea nchini Hispania katika timu ya Tenerife.