
Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe na Mbwana Samatta
Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa Samatta amefanya jambo kubwa kwa kuzingatia Ubelgiji ni moja ya mataifa makubwa tena yanayofanya vizuri kwenye mchezo wa soka duniani.
''Samatta amefanikiwa kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania, ni shujaa ambaye mchango wake ni mkubwa na tunajaribu kuona ni vipi Samatta anaweza kuwa Balozi wa vivutio vyetu vya utalii, Sanaa na Michezo'', amesema.
Mbwana Samatta ambeye ni mchezaji wa zamani wa Simba, TP Mazembe na mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016, mpaka sasa ni kinara wa mabao kwenye ligi kuu ya Ubelgiji akiwa amefunga magoli 20.
Samatta alijiunga na Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ambapo mwaka huo pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ndani Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa.