Jumapili , 20th Aug , 2017

Mshambuliaji mpya wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Wazir Junior, ameweka wazi kuwa yupo tayari kwa mapambano.

 

Wazir amesema kuwa moja ya malengo yake ni kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) msimu 2017/2018.

"Kuanza kwa msimu mpya 2017/2018, kwangu mimi nimejipanga kuisaidia timu yangu kuwa mabingwa msimu ujao na mwenyewe kucheza vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu kwani ushirikiano wetu ndio utatupa hamasa kama wachezaji ya kufanya vizuri na kuisaidia timu yetu kubeba ndoo (ubingwa)" - Wazir.

Aidha Wazir ni kati ya washambuliaji wanaokuja kwa kasi, amesajiliwa Azam FC msimu huu akitokea Toto African ya Mwanza na alifanikiwa kufunga mabao saba msimu uliopita.

Azam FC inatarajia kufungua msimu mpya wa ligi Jumamosi ijayo Agosti 26 mwaka huu kwa kukipiga dhidi ya Ndanda, mtanange unaotarajia kufanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.