
Licha ya hali ya ugonjwa iliyokuwa ikimkabili nyota huyo iliyosababishwa na kuonja chakula cha mbwa wake amepata ushindi wa seti mbili kwa kumshinda mpinzani wake Christina Mchale kwa 7-6 na 6-1.
Muingereza Johanna Konta akaputwa nje ya michuno hiyo baada ya kuchapwa na Misaki Doi wa Japan kwa seti ya kwanza alishinda kwa 4-6 kisha akapoteza kwa 7-5 na 6-2.
Kwa upande wa wanaume Andy Murray amesonga mbele baada ya kumshinda Jeremy Chardy kwa 6-0 6-4, hivyo Murray atachuana na David Goffin, aliyemshinda Tomas Berdych kwa 6-0 6-0.
Roger Federer akatupwa nje na Dominic Thiem kwa kupoteza kwa 7-6 (7-2) 6-4.Thiem atakutana na Kei Nishikori, hatua inayofuata .
Nae nyota namba moja kwa ubora Novack Djokovic alimshinda Tomaz Belluci kwa kwa seti 6-3, 6-2 huku akipoteza seti ya kwanza kwa 0-6, Djockovic atachuana na Rafael Nadal aliyemshinda Nick Kyrgios kwa 6-2 na 6-4.