Ijumaa , 14th Nov , 2014

Serikali imekiri kuwa makato yanayokatwa kwa vilabu vya mpira wa miguu nchini Tanzania ni makubwa kiasi ambacho kinapelekea vilabu hivyo kukosa mapato yanayostahili kwa ajili ya maendeleo ya vilabu hivyo.

Akijibu swali la Mbunge wa Tabara ambae pia aliwahi kuwa Rais wa Klabu ya Simba Mh. Ismail Aden Rage, Naibu waziri wa Michezo na Utamaduni Mh. Juma Nkamia amesema serikali itakaa na bodi ya ligi ili kulitatua tatizo hilo.

Mh. Nkamia ameongeza kuwa kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kuweza kupunguza mapto hayo ili kuweza kusaidia kukuza vilabu vya soka nchini Tanzania na kuweza kujiendesha vyenyewe kwa kiasi kikubwa.