Alhamisi , 9th Jul , 2020

Kocha wa Barcelona Quique Setien amepongeza uwezo wa mshambuliaji wake Luis Suarez ambaye aliifungia timu yake bao pekee na la ushindi katika mchezo wa jana dhidi ya Espanyol ambao umeendelea kuwapa matumaini ya kutetea taji la La Liga msimu huu.

Luis Suarez(kati kati pichani) akiwa akishangilia na Antoine Griezma(Kulia) na nahodha wake Lionel Messi(Kushoto) katika picha.

Setien amesema mshambuliaji huyo amekamilika na amekua akifanya majukumu yake ipasavyo kiasi cha kuipa timu matokeo muhimu pale yanapohitajika.

Suarez raia wa Uruguay alifunga bao hilo dakika ya 56, ambalo lilikua ni la 15 katika msimu huu wa La Liga, pia limemfanya awe mfungaji bora wa tatu wa muda wote wa Barcelona baada ya kufikisha idadi ya mabao 195 nyuma ya vinara Lionel Messi mwenye mabao 630 na Cesar Ridrigues aliyefunga mabao 232.

Ushindi wa Barcelona umefanya wafikishe alama 76, alama moja nyuma ya vinara Real Madrid ambao wana alama 77 huku wakisalia na michezo mitatu  kumalizia msimu.

Kwa upande wa Espanyol ni rasmi wameshushwa daraja kwa kuwa alama 24 walizonazo na idadi ya mechi zilizosalia hazitatosha kuwanusuru hata kama watashinda yote.