
Kikosi cha Yanga
-'Cannavaro' ambaye amestaafu soka.
Akizungumza na www.eatv.tv Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema sababu kubwa ya mchezo huo kuchezwa mkoani Morogoro ni kutokana na wao, kuweka kambi hapo ya kujiandaa na michuano ya ligi.
"Tunacheza mechi ya kirafiki na Mawenzi FC lakini hii mechi ni mwanzo wa kumuaga Cannavaro kama mnavyoelewa anastafu mpira, tuliweka kambi Morogoro kwa hiyo tukaona bora tuanze na hapa moja kwa moja. Naomba mashabiki na wapenzi wa Yanga wafahamu kwamba mchezo huu sio wa kutambulisha wachezaji bali ni wa kumuaga Nahodha wetu", amesema Nyika.
Cannavaro alijiunga na Yanga tangu mwaka 2006 alipokuwa akitokea timu ya Malindi ya Zanzibar hadi mwaka huu 2018 anapoondoka, ameshinda jumla ya mataji 15, kati ya hayo, mataji nane (8) ya ligi kuu bara, mataji manne (4) ya ngao ya jamii, mawili ya Kagame na moja ya michuano ya kombe la shirikisho .
Msikilize hapa chini Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika akizungumza zaidi juu ya mchezo huo.