Kiungo wa Simba Mzamiru Yassini wa kulia ni moja ya wachezaji watakaokosekana kwenye mchezo dhidi ya Biashara United kesho
Kocha mkuu wa Simba Pablo Franco Martin amethibitisha kuwakosa nyota kadhaa kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu, na wachezaji hao ni Chris Mugalu, Taddeo Lwanga, Kibu Denis wachezaji hawa ni majeruhi wa muda mrefu wanaungana na Sadio Kanoute ambae pia ana majeruhi wachezaji wengine watakaokosekana kwenye kikosi cha wekundu wa msimbazi ni Aishi Manula, Mzamiru Yassini na Larry Bwalya.
Kwa upande mwingine kocha huyo Raia wa Hispania ameweka wazi kuwa wachezai wake wanauchovu kutokana na safari yao ya kurudi kutoka nchini Morocco, na anaamini mchezo huo dhidi ya Biashara utakuwa mgumu lakini watapambana ili kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi,
‘’Utakuwa mchezo mgumu kwetu, tumewaangalia Wana timu nzuri na iliyojipanga vizuri kitimu tumewaona wakicheza vizuri kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Yanga, lakini niliwoana wakicheza na Azam na Namungo kwenye michezo ya ligi pia. kwa Sasa tunajiandaa na mchezo wa kesho hatuna muda maana unaweza kuona jinsi wachezaji walivyo na uchovu wa Safari lakini tutapambana kufanya vizuri.” Amesema Pablo
Mchezo huu utachezwa kesho Saa 1:00 Usiku ukiwa ni mchezo wa kiporo wa raundi ya 16, Simba wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa wanazidiwa alama 11 na Yanga SC wenye alama 42 ambao ndio vinara wa Ligi lakini yanga wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Simba walio nafasi ya pili wakiwa na alama 31.




