(Baadhi ya wachezaji wa Simba SC wakijiandaa kusafiri)
Mabingwa hao watetezi wa ligi Kuu NBC Tanzania, wataweka kambi ya siku 4 nchini Morocco kabla ya kuwakabiri wenyeji RS Berkane kwenye mchezo wa mzunguko watatu wa kundi D michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika Februari 27, 2022.
Simba imetokea nchini Niger kwasababu walikuwa na mchezo wa mzunguko wapili wa kundi hilo dhidi ya US Gandermarie ambao Simba alilazimisha sare ya 1-1 Ugenini kwa goli la Bernard Morrison dakika ya 84.
Simba SC ndiyo vinara wa kundi D wakiwa na alama 4 ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo katika kundi hilo, RS Berkane wapili wana alama tatu, ASEC Mimosas alama 3 huku US Gandermarie akishika mkia akiwa na alama 1.



