Jumanne , 6th Dec , 2016

Shirikisho la Soka nchini (TFF) limetangaza ratiba ya ligi kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili unaotarajia kuanza kutimua vumbi Desemba 17 mwaka huu na kuhitimishwa Mei 06, mwaka 2017 ambapo Simba na Yanga wamepangwa kukutana Februari 18, 2017.

Mechi ya Yanga na Simba mzunguko wa kwanza

Katika siku yake ya kwanza ya Desemba 17, mechi nne zitapigwa ambapo mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa JKT Ruvu, Mbeya City itaikaribisha Kagera Suga, Ruvu Shooting itaialika Mtibwa Sugar na Toto Africans watakuwa wageni wa Mwadui FC.

Kesho yake Desemba 18, Mbao FC itakuwa mwenyeji wa Stand United, Ndanda Fc itaikaribisha Simba SC, African Lyon itakuwa mwenyeji wa Azam Fc huku majimaji ikialikwa na Tanzania Prisons.

Katika mzunguko huo wa pili wa ligi kuu, watani wa jadi Simba na wamepangwa kukutana siku ya Jumamosi ya Februari 18.

TFF imesema kuwa timu za Azam FC, JKT Ruvu na Ruvu Shooting zitatumia Uwanja wa Uhuru katika michezo watakayocheza dhidi ya Yanga au Simba SC.

Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema, maamuzi hayo yamefikiwa na wao TFF pamoja na bodi ya ligi kuhusu timu hizo kutumia Uwanja wa Uhuru watakapokutana na Simba au Yanga mara baada ya kujadiliana kwa kuzingatia kanuni ambayo inaruhusu na vilabu hivyo vilishapewa taarifa juu ya maamuzi hayo

Ratiba kamili hii hapa