Manyika Jr, kipa wa Simba aliyedaka leo
Jambo kubwa linaloweza kusababisha hofu kwa benchi la ufundi, mashabiki na hata wachezaji ni timu hiyo kuwa na uwezo wa kucheza lakini ikiwa haipati mabao ya kutosha licha ya kupata ushindi na kuzua maswali endapo timu hiyo itaendelea kupata ushindi katika michuano hiyo.
Katika mchezo wa leo ambao imetulizwa na URA ambao ndiyo mabingwa watetezi, Simba imeshindwa kupata bao hata lile moja ililopata katika michezo kadhaa iliyopita, licha ya kuonesha kandanda safi katika mchzo uliokuwa ni wa vuta nikuvute.
Simba ambayo leo kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi imemchezesha golikipa wake Manyika Peter, imekutana na upinzani mkali lakini imefanikiwa kuzuia moto wa wshambuliaji hatari wa URA wakiongozwa na Bogota, kufuatia ukuta imara uliowekwa na Method Mwanjale na Abdi Banda na mwisho wa mchezo Method Mwanjale aliibuka mchezaji Bora.
Mwingine aliyepata nafasi ya kucheza leo ni Haji Ugando aliyeingia dakika ya 87 kuchukua nafasi ya Shiza Kichuya, ambaye licha ya makali yake katika ligi, hajafunga bao lolote katika michuano hii.
Jambo linguine linatia hofu Simba ni matokeo ya ushindi wa 3-1 iliyopata leo Jang’ombe Boys dhidi ya KVZ na kufanya timu hiyo ya Zanzibar ifikishe point 6 na kuikaba Simba ambayo sasa imefikisha point 7 ikiongoza kundi hilo.
URA baada ya kufungwa juzi na Jong’ombe Boys, imefikisha point 4 na hivyo timu zote katika kundi hilo zina nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali isipokuwa KVZ ambayo tayari imefungwa mechi zote 3.





.jpg?itok=0CrdpE0P)