Simba SC kuifata Kaizer Chiefs kesho

Jumatatu , 10th Mei , 2021

Klabu ya Simba SC itaondoka nchini kesho Mei 11, 2021 kuelekea Afrika ya Kusini, kikosi hicho kitacheza mchezo wa klabu bingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs Mei 15, 2021.

Kikosi cha Simba SC

Taarifa iliyotolewa na mabingwa hao wa Tanzania bara imeeleza,

''Kikosi cha mabingwa wa nchi kitaondoka alfajiri ya jumanne Mei 11, 2021 (saa 9:45) kuelekea Afrika Kusini kupitia Kenya tayari kwa mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa siku ya Jumamosi Mei 15, 2021''

Simba SC ilitinga hatua robo fainali baada ya kumaliza vinara wa kundi A wakiwa na alama 13 baada ya kushinda michezo 4 wametoka sare mchezo mmoja na walifungwa mchezo mmoja, Wekundu wa msimbazi walimaliza vinara wa kundi hilo mbele ya mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri, AS Vital na AL Merrikh.

Na wanaanzia ugenini kutika mchezo huu kutokana na faida za kikanunu za kumaliza vinara wa kundi, kwa mujibu wa kanuni za CAF timu zinazomaliza kama vinara wa makundi zinapewa faida ya kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani kwenye hatua ya robo fainali.