Jumapili , 25th Jul , 2021

Klabu ya soka ya Simba SC sasa imetwaa ubingwa wa ASFC kwa mara ya pili mfululizo na ya tatu katika historia ya michuano hiyo na ndio klabu iliyotwaa mara nyingi zaidi.

Wachezaji na viongozi wa Simba SC wakishangilia ubingwa

Simba SC imetwaa ubingwa huo baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Yanga SC leo Julai 25, 2021 kwenye mchezo wa fainali ya kombe hilo la shirikisho Tanzania msimu wa 2020-21 iliyopigwa kwenye dimba la Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Goli pekee la Simba SC limefungwa na Taddeo Lwanga dakika ya 79 kwa kichwa akiunganisha kona iliyopigwa na Luis Miquissone.

Simba imebeba ubingwa huo katika misimu ya 2016-17, 2019-20 na 2020-21.