Jumatatu , 8th Apr , 2019

Hii leo April 8, uongozi wa klabu ya Simba umetuma barua ya malalamiko yao kwa Shirikisho la Soka Barani Afrika baada ya kupewa taarifa ya kubadilishiwa waamuzi.

Simba na CAF

Simba imefikia hatua hiyo baada ya kupokea barua kutoka CAF kuwa waamuzi ambao walipangwa kusimamia mchezo wa marudio kati ya TP Mazembe na Simba utakaopigwa DR Congo wikiendi hii wamebadilishwa kutokana na sababu za kiufundi.

Barua hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Creacentius Magori, imeendelea kusema kuwa mabadiliko hayo hayakupaswa kufanyika bila kuwa na mawasiliano na wahusika, huku ikionesha wasiwasi wao juu ya waamuzi walioteuliwa kuwa na uhusiano wa karibu na taifa la Congo kwakuwa wao ni raia wa Zambia.

Imetoa pendekezo la kurejeshwa kwa waamuzi wa awali ili kuepusha mgongano wa kimaslahi. 

Simba na TP Mazembe zitapambana katika mchezo wa marudio wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika mjini Lubumbashi, ambapo mchezo wa kwanza uliofanyika Jumamosi iliyopita, ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.