Jumanne , 26th Oct , 2021

Klabu ya Simba imethibitisha kuridhia ombi la Kocha Mkuu, Didier Gomnes da Rosa la kuachana na Simba kuanzia leo baada ya tathmini na majadiliano ya kina pande zote zimeafikiana kwa mujibu wa Mkataba na manufaa ya wote.

Didier Gomes da Rosa

Kutokana na hatua hiyo, aliyekuwa Kocha Msaidizi, Thierry Hitimana ndiye atakuwa Kocha Mkuu wa Simba katika kipindi hiki cha mpito akisaidiwa na Selemani Matola.

Aidha, Klabu imefanya mabadiliko madogo katika benchi la ufundi kwa kusitisha mikataba ya aliyekuwa Kocha wa Makipa, Milton Nienov na Kocha wa Viungo, Adel Zrane.

Klabu ya Simba inamshukuru Kocha Gomes na wenzake kwa mafanikio waliyoyapata katika kipindi walichoitumikia Simba na kuwatakia heri katika majukumu yao mengine waendako.