
Wachezaji wa Simba kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Asante Kotoko
Bodi hiyo ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba imeteua kamati ya uchaguzi yenye watu watano kwaajili ya kusimamia uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika siku chache zaijazo.
Walioteuliwa kwenye kamati ni Mwenyekiti Boniphace Lyamwike, Wakili Steven Ally ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti, Issa Batenga atakayekuwa Katibu pamoja na wajumbe wawili ambao ni Iddy Mbita na Richard Mwalwiba.
Kamati hiyo itatangaza tarehe ya uchaguzi hivi karibuni na kuitisha uchaguzi wa wajumbe wa Bodi ya Simba Sports Club Company Limited ambao watachaguliwa kwa mujibu wa ibara ya 27 ya katiba ya Simba.
Julai 24 mwaka huu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) liliipa Simba siku 75 kuhakikisha inafanya uchaguzi wake kwani viongozi waliopo sasa wamemaliza muda wao. Simba sasa ipo chini ya kaimu Rais Salim Abdallah na Kaimu Makamu wa Rais Iddi Kajuna.