
Mtendaji Mkuu mpya wa Simba Senzo Masingizi
CEO anayeondoka Crescentius Magori, amemtambulisha rasmi mtendaji huyo mpya leo, Septemba 7, 2019 kwenye mkutano na wanahabari.
Baada ya utambulisho CEO huyo mpya ambaye imeelezwa kuwa amefanya kazi na vilabu kama Orlando Pirates, Platinum Stars FC pamoja na chama cha soka Afrika Kusini, amesema anamtambua kazi ngumu iliyombele yake lakini amejipanga kuifanya vyema.
''Najua Simba ni taasisi kubwa, ina majukumu mengi ya kuyasimamia, ina malengo makubwa ya kuyatimiza na mimi nipo tayari kufanya hivyo na uongozi wangu utafanya kazi kwa misingi ya uhuru na uwazi mkubwa'', amesema.
Aidha Senzo Masingizi amesema ataendelea kujifunza Kiswahili ili kurahisisha utendaji kazi wake, lakini pia kwa kuwa tayari Lugha hiyo inatumika kwenye Jumuiya ya SADC.