Singida United yaingiza Waserbia

Jumamosi , 12th Jan , 2019

Uongozi wa klabu ya Singida United umewatambulisha rasmi makocha wake kwaajili ya kuimarisha benchi lake la ufundi.

Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga akiwatambulisha makocha wapya

Maamuzi hayo yametolewa katika mkutano na waandishi wa habari  ambapo imewatangaza makocha hao wawili raia wa Serbia.

Katika taarifa yake rasmi kupitia ukurasa wa Twitter, Singida United imeandika, "uongozi wa klabu hii leo umeamua kuimarisha benchi la ufundi kwa kuwaajili makocha wawili ambao ni raia wa Serbia na wamewahi kufanya kazi hapa nchini kwa mafanikio makubwa. Kocha Mkuu: Popadic Dragan, Kocha Msaidizi: Dusan Momcilovic".

Hatua hiyo imekuja baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Hemed Morocco kuachana na klabu hiyo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi na uongozi wa klabu.

Singida United inajiandaa kushiriki michuao ya Sport Pesa Super Cup pamoja na ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika ligi kuu, Singida United inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 24.