Ijumaa , 20th Mei , 2022

Marcus Smart alirejea kutoka majeruhi ya mguu na kuisaidia timu yake Boston Celtic kupata ushindi dhidi ya Miami Heat na kufanya matokeo kuwa sare ya 1-1 katika mfululizo wa mechi za fainali ukanda wa Mashariki.

Marcus Smart akionysha ubora wake

Smart alifunga alama 24,asisti 12 na rebound 9 wakati Celtics ikishinda kwa alama 127-102 kwnenye mchezo uliofanyika katika Jiji la Florida.

Nyota huyo alishuhudiwa akifunga kwa mitupo ya alama tatu mara tano (zilizokusanya alama 15 )katika mchezo hu.

Jayson Tatum ambaye ndiye mfungaji bora hadi sasa wa Boston Celtics alifunga alama 27 naye Jimmy Butler akaifungia Miami alama 29 akiwa ndiye kinara wa ufungaji kwa timu hiyo.

Jayson Tatum top-scored for the Celtics with 27 points, while Jimmy Butler led the Heat with 29.

Akizungumza baada ya mchezo huo,Smart ambaye ni mchezaji bora wa ulinzi wa mwaka katika NBA amesema anajisikia vizuri kujiunga na wenzake kupigania ushindi dhidi ya Miami Heat na anaamini wanaweza kufanya vizuri.

Mchezo wa tatu baina ya Miami na Boston utapigwa siku ya Jumamosi alfajiri.