Jumatatu , 27th Apr , 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kuweka kambi nchini Ethiopia kujiandaa na mechi dhidi ya Misri ambayo ni michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Rais wa shirikisho la soka nchini TFF, Jamal Malinzi amesema, michuano mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa June 13 mwaka huu ambapo katika kundi hilo Tanzania imepangwa na nchi za Misri, Nigeria na Chad.

Malinzi amesema, lengo hasa la kuweka kambi Ethiopia ni kuweza kuwaweka wachezaji katika hali nzuri ya kimichezo ili kuweza kupambana na kushinda katika mechi hiyo ya awali.

Katika michuano hiyo, timu mbili zilizomaliza hatua hii ya awali kwa rekodi bora kuliko nyingine zitaungana na wenyeji timu ya taifa ya Gabon kukamilisha timu 16 zitakazoshiriki michuano ya AFCON mwaka 2017.