
Kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars”
Agosti 28 Stars ilipoteza mechi ya kwanza ikifungwa bao 1-0 na Uganda, Uwanja wa Benjamin Mkapa,hivyo inahitaji ushindi kwenye mchezo huo, ili kuendelea kusonga mbele kwenye mchezo huo.
Stars inaondoka nchini ikiwa na kocha mpya, Mzambia Hanoor Janza aliyechukua mikoba ya Kim Poulsen aliyefutwa kazi baada ya kupoteza mechi ya kwanza na Uganda.
Janza amemuongeza straika John Bocco ndani ya kikosi chake na amemuelezea kwamba kutokana na uzoefu wake ataleta tija kwenye timu.
"Bocco ni mzoefu na mchezaji mzuri, uwepo wake kwenye timu utasaidia sana, hiyo ndio sababu kubwa ya kumjulisha,Bado anahitajika kulitumikia taifa lake," amesema.
Mbali na kumzungumzia Bocco amesema wachezaji wote wapo sawa na anaamini watafanya kazi nzuri kwenye mchezo huo wa marudiano.