
Mchezaji kiraka wa Taifa Stars, Erasto Nyoni akiwa katika majukumu ya kitaifa.
Nyoni hakuwepo kambini wakati Taifa Stars ikijiandaa na michuano hiyo kwakuwa alielekea nyumbani kwao mkoani Ruvuma kutatua matatizo ya kifamilia lakini alishindwa kurejea kikosini kwa wakati.
Taifa Stars iliondoka nchini alfajiri jana na kuwasili Cameroon tayari kwa matayarisho ya mwisho ya michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi kesho Januari 16, 2021.
Tanzania itaanza kampeni zake za kuwania kufika mbali katika michuano hiyo ikitokea kundi D kwa kukipiga dhidi ya Zambia Januari 19 mwaka huu.