Jumanne , 22nd Sep , 2020

Katibu wa klabu ya Mbeya City Emmanuel Kimbe amesema kuwa kitendo cha timu hiyo kucheza mechi tatu ambazo ni sawa na dakika 270 pasi na kupata walau bao moja katika Ligi Kuu Tanzania Bara VPL si suala jema kwa afya ya timu hiyo.

Mshambuliaji wa Yanga, Tuisila Kisinda (Kushoto) akijaribu kumpita mlinzi wa Mbeya City, Hassan Mwasapili (Kushoto) katika mchezo wa VPL uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa .

Kimbe ameitoa kauli hiyo hii leo alipozungumza na Kipenga ya East Africa Radio kwa njia ya simu amesema mwalimu Amri Saidi analifanyia kazi hili.

"Kwahiyo Mwalimu tumemkumbusha na anajua hilo kwamba tumecheza mechi tatu bila goli kwahiyo kuna uhitaji wa kufanyia kazi eneo la ushambuliaji ili hali iweze kuwa nzuri" amesema Emmanuel Kimbe

Aidha, Katibu huyo amekanusha maneno ya uvumi yanaoendelea mitandaoni na midomoni mwa wapenzi wa soka nchini kuwa viongozi wa Mbeya City wamempa Mwalimu wao Amri Saidi mechi mbili tu za kitimoto, ile dhidi ya Namungo na dhidi ya Prisons

"Ninachojua mwalimu wetu ni Amri Saidi na tuna mipango nae katika mechi zinazofuata. Niwaombe tu msizipokee taarifa zozote ambazo hazijatoka kwenye vyanzo rasmi vya klabu hiyo" amesema Emmanuel Kimbe

Hata Katibu huyo amewataka wapenzi na washabiki wa timu hiyo hususani wale wa mkoani kwao watulie na kuiunga mkono timu hiyo "kubwa ni kutulia katika kipindi hiki, turekebishe tupate matokeo tuondokane na hali tuliyonayo ili watu wa Mbeya wapate kufurahi." Emmanuel Kimbe

"Kufanya vibaya hakumaanishi kuna shida ni matokeo tu hamna tatizo lolote kutoka kwa hayo yanayosemwa." Emmanuel Kimbe Katibu Mbeya City

"Kwahiyo Mwalimu tumemkumbusha na anajua hilo kwamba tumecheza mechi tatu bila goli kwahiyo kuna uhitaji wa kufanyia kazi eneo la ushambuliaji ili hali iweze kuwa nzuri." Emmanuel Kimbe Katibu Mbeya City

"Kubwa ni kutulia katika kipindi hiki, turekebishe tupate matokeo tuondokane na hali tuliyonayo ili watu wa Mbeya wapate kufurahi." Emmanuel Kimbe Katibu Mbeya City

"Ninachojua mwalimu wetu ni Amri Saidi na tuna mipango nae katika mechi zinazofuati." Emmanuel Kimbe Katibu Mbeya City.