
Wachezaji wa kikosi cha Tanzanite
Tanzanite imefuzu raundi ya tatu ya michezo ya kufuzu kombe la Dunia kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20 barani Afrika baada ya kuiondoa Burundi kwenye raundi iliyopita kwa ushindi wa jumla wa michezo miwili kwa mabao 4-3.
Mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulichezwa Jijin Dar es salaam Tanzanite iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, na mchezo wa mkondo wa pili uliochezwa Jumamosi Disemba 18 timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Kwenye mchezo wa Jumamosi kikosi cha Tanzania kilicheza kikiwa na wachezaji 8 tu uwanjani baada ya wachezaji 11 kuripotiwa kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona pamoja na viongozi 5.
Tanzanite watakuwa wenyeji wa Ethiopia kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya tatu utakaochezwa kati ya Januari 21-23, 2022 na mchezo wa mkondo wa pili utachezwa kati ya Februari 4 -6, 2022, ni timu 8 ndio zilizosalia na ni matiafa mawili tu ndio yatakayowakilisha bara la Afrika kwenye fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Costa Rica mwaka 2022.